Hakuna kanuni au mbinu moja tu ya mafanikio ambayo unaweza ukatumia hadi kumfanikisha mtu moja kwa moja. Kwa kawaida zipo kanuni au siri nyingi sana ambazo zinaweza kumfanya mtu akaweza kufanikiwa.
Leo katika makala haya kwa ufupi, naomba nikushirikishe siri tatu muhimu za kimafanikio ambazo unaweza kuzitumia leo na ukaishi maisha ya ushindi na mafanikio kwa upande wako. Ni siri ambazo unatakiwa uzitumie kila siku.
Siri Ya 1, KUWEKEZA.
Umeshawahi kujiuliza ni kipi au kitu gani kinachofanya maisha yako kuwa bora? Hakuna kitu kingine kinachoweza kufanya maisha yako yakawa bora na maana zaidi ya KUWEKEZA.
Kila wakati angalia na chunguza ni kipi ambacho unakiwekeza katika maisha yako. Usiwe mtu wa kutaka kupata mafanikio tu wakati hujawekeza. Ukiwa unataka kupata tu mafanikio bila kuwekeza utajiumiza bure.
Mafanikio yote yanaanza na kuwekeza kwanza. Hakuna kinyume cha hapo. Kabla hujatamani mafanikio ya namna fulani, jiulize kwanza umewekeza nini ili kuyapata mafanikio hayo?
Ukishagundua hujawekeza kitu, kaa pembeni, kaa kimya, usijiumize kwa kitu chochote, maana huko itakuwa ni kupoteza muda wako bure. Wekeza kwanza, na utapata maisha unayoyataka. Hii ni siri namba moja ya kukufanya ukawa mshindi.

Siri Ya 2, TENGENEZA FURSA.
Mbali na kuwekeza, siri nyingine ni kwamba kuanzia siku ya leo, tambua unayo nafasi kubwa ya kutengeneza fursa kubwa ya mafanikio. Kuanzia siku ya leo pia unayo nafasi ya kutengeneza maisha yako na kuwa bora kwa jinsi unavyotaka wewe yawe.
Mpaka hapo pia najua umeshajifunza sana juu ya jambo lipi linaweza kukupa mafanikio na jambo kipi ambalo haliwezi kukupa mafanikio. Kwa kujua hivyo tu, chukua hatua kwa kufanyia kazi mambo hao siku ya leo.
Siku ya leo ni ukurasa mpya wa mafanikio yako. Je, jiulize umechagua kuandika nini katika ukurasa huu? Amua kuanzia leo na siku zote zinazofuata kuwa siku za mafanikio makubwa kwako kimaisha.
Amua kutumia kila dakika, kutaka kuweza kufanikisha yale yaliyo bora katika maisha yako. Kumbuka siku ya leo ni nafasi pekee kubwa uliyonayo wewe kuweza kutengeneza maisha yako na kuwa ya mafanikio makubwa.
Siri Ya 3, UNAWEZA.
Kuwekeza na kutengeneza fursa peke yake haitoshi, ila ila wakati fikiria unaweza katika kile unachokifanya. Endelea kufikiria hivyo unaweza huku ukiangalia namna ya kuweza kuchukua hatua.
Kila wakati tenda kwa kujua kama unaweza, hata kama hauna uhakika sana wa hicho unachokifanya, lakini fanya kwa kujiamini unaweza.
Kila wakati weka hisia na mtazamo wa kuweza katika akili yako na katika hali ya kushangaa utajikuta unaweza.
Kama utaendelea katika hali hiyo ya kufiria unaweza..ya kufikiria unaweza kuchukua hatua,. ya kujenga matazamo ninaweza,.utajikuta unajenga nguvu kubwa ya mafanikio.
Endelea kufanya maisha yako kuwa bora zaidi  kwa KUFIRI, KUTENDA NA KUJENGA MTAZAMO wa kuweza kwenye maisha yako.
Hizo ndizo siri tatu muhimu za kukufikisha kwenye maisha ya ushindi ambazo unatakiwa uzitumie karibu kila siku kwenye maisha yako.

Tupia Comments: