TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutokana na kifo cha Dk Elly Macha Machi 31, mwaka huu.
Kutangazwa kwa nafasi hiyo kumekuja baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuijulisha Tume kuhusu kuwepo kwa nafasi hiyo. Akitangaza nafasi hiyo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji wa Rufaa, Semistocles Kaijage alisema taratibu ya kujaza nafasi hiyo zinaendelea.
Jaji Kaijage alisema katika taarifa hiyo kuwa maandalizi hayo, yanafanyika kwa kuzingatia Ibara ya 78 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia ya mwaka 1977. Kwa upande wake, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alikiri kupokea barua ya Nec na kusema kuwa taarifa zaidi kuhusu kinachoendelea katika matayarisho ya kujaza nafasi hiyo, zitatolewa baadae
Tupia Comments: