Baada ya wiki za majibizano makali kati ya Marekani na Korea Kaskazini, Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaweza kufurahia kukutana na Kim Jong Un. Lakini ilikuwaje hadi mambo yakafikia hapa?
Nini kimebadilika chini ya Trump?
Tishio: Wamarekani wanaamini kwamba Korea Kaskazini tayari ina teknolojia ya kurusha makombora ya nyuklia hadi Japan na Korea Kusini. Wanakadiria kwamba taifa hilo litakuwa na uwezo wa kurusha makombora hadi Marekani katika miaka michache ijayo.
Kwa hivyo, Korea Kaskazini kwa sasa inachukuliwa kama tishio kwa usalama wa taifa la Marekani, na si tishio tu kwa washirika wake Asia mashariki. Hii ndiyo inayoongeza dharura katika haja ya kushughulikia tishio hilo.
Maneno makali: Hatua ya kijeshi ndiyo ambayo imefikiriwa zaidi kwa muda mrefu. Lakini hakuna serikali ya Marekani ambayo imekuwa wazi kuhusu hilo kuliko serikali ya Trump. Hii sana ni kutokana na mtindo wa uongozi wa Bw Trump na imani kwamba tishio la Korea Kaskazini limezidi.
Ubabe wa kijeshi: Majira ya kuchipuza huwa ya wasiwasi sana rasi ya Korea, sana kwa sababu ndio wakati Korea Kaskazini husherehekea siku muhimu katika taifa hilo. Ni kipindi hiki ambapo taifa hilo hufanyia majaribio silaha mbalimbali. Aidha, wakati huu pia ndio Marekani hufanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja an Korea Kusini.
Lakini mwaka huu, utawala wa Trump umeongeza nguvu katika kuonyesha ubabe wake kijeshi, kwa kutuma nyambizi yenye uwezo wa kurusha makombora pamoja na meli kubwa ya kubeba ndege za kivita. Kulikuwa na utata kuhusu wapi meli hiyo kubwa ilikuwa inaelekea awali, lakini baadaye ilithibitishwa kwamba ilikuwa inaelekea rasi ya Korea. Utata huo huenda ulichangia kupunguza uwezo wake kama onyo kali kwa Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini: Pyongyang kwa muda mrefu imeamini kwamba inahitaji silaha za nyuklia ili kujilinda, na imekuwa tayari kukabiliana na vitisho na adhabu kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Kim Jong Un ameonyesha kujitolea kwake, kinyume na babake na babu yake, kupuuza msimamo na maoni na mshirika pekee mkuu wa Korea Kaskazini, China.
Kiongozi wa mashauriano wa zamani wa Marekani Chris Hill anasema Kim Jong il (babake Kim Jong-un) alijali sana yale ambayo wengine walifikiria, na hasa Wachina. Lakini mwanawe Kim Jung Un hajali wasemayo watu.
China: China imeonekana kutamaushwa na mshirika wake Korea kaskazini na ina wasiwasi kuhusu taifa hilo kuendelea kujiimarisha kwa silaha.
Tayari China imeanza kukaza vikwazo vilivyowekewa Pyongyang na Umoja wa Mataifa, sana kuhusu uagizaji wa makaa ya mawe.
Lakini labda ina wasiwasi zaidi kwamba kujionyesha kijeshi kwa Trump kutazidisha uhasama na wasiwasi eneo hilo.
Aidha, China haijafurahishwa na hatua ya Trump kuendelea kukariri kwamba Beijing ina nafasi ya kipekee ya kuweza kuidhibiti Pyongyang.
Katika kilichoonekana kama hatua ya kujibu shinikizo kutoka kwa Marekani, magazeti ya China yalichapisha taarifa zenye msimamo mkali dhidi ya Korea Kaskazini.
Kumekuwa pia na ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Beijing na Washington.
Waziri wa ammbo ya nje wa Marekani Rex Tillerson anasema Beijing ametishia kuiwekea vikwazo vyake binafsi Pyongyang iwapo itafanya jaribio la sita la silaha za nyuklia.
Mambo ambayo hayajabadilika
Njia za kukabili Korea Kaskazini: Bado hakuna njia moja mwafaka.
- Kushambulia na kulipua viwanda, vinu na silaha za nyuklia za Korea Kaskazini ni hatua ambayo inaweza kusababisha uvamizi mkubwa wa kulipiza kisasi dhidi ya Korea Kusini. Uvamzii kama huo unaweza kutishia raia 10 milioni wanaoishi Seoul na wanajeshi 28,000 walio nchini humo.
- Vikwazo vya Umoja wa Mataifa pia havijafanikiwa kufikia sasa. Kimsingi, huwa vinadhoofishwa ili wahusika wakuu waafikiane, na huwa kuna mapengo mengi katika utekelezwaji wake. Marekani imekuwa ikiomba kuwe na marufuku dhidi ya kuiuzia wala kununua bidhaa za Korea kaskazini. Lakini hatua kama hiyo itahitaji kufuatiliwa kwa karibu na pia ushirikiano wa jamii ya kimataifa kama ilivyofanyika kwa Iran.
- Mazungumzo yamejaribiwa awali lakini Pyongyang imekuwa ikiyatumia kujitetea ipate misaada ya chakula, na baada ya kupata hayo huwa inarejea kustawisha silaha zake za nyuklia. Wataalamu wa Kotea Kaskazini wanaamini taifa hilo halifai kamwe kusalimisha silaha zake za nyuklia, jambo ambalo limekuwa likiitishwa na Marekani kama sharti kabla ya mazungumzo kuanza. Huwa wanatazama wazo la kusitishwa kwa uundaji wa silaha kama njia ambayo labda inawezekana kwa kiwango fulani.
Tillerson anasema kumalizwa kwa silaha za nyuklia Korea Kaskazini bado litakuwa ndilo lengo kuu, lakini bado hajaeleza masharti ya kutimizwa kabla ya mazungumzo kuanza.
Njia za kukabili Korea Kaskazini: Kwa kweli, njia hizi hazijabadilika sana. Serikali ya Trump imekuwa ikidai kwamba kumekuwa na mabadiliko.
Lakini njia zinazotumiwa - kuitisha vikwazo zaidi vya kiuchumi, kuitaka China imdhibiti jirani yake huyo na kusubiri Korea Kaskazini ibadilike kutokana na shinikizo - ni njia ambazo zinafanana sana na zilizotumiwa na Barack Obama.
Tofauti pekee inaonekana kuwa kutokuwa na subira sana na Korea Kaskazini, na kutumia shinikizo za kidiplomasia na vitisho, ikiwa ni pamoja na kutishia kuishambulia Pyongyang kijeshi.
Pamoja na China, Trump amekuwa akijaribu pia kushawishi mataifa ya Afisa Mashariki kuitenga Korea Kaskazini.
China: China inaonekana kuwa tayari kuishinikiza Pyongyang, lakini si sana. Bado hakuna dalili kwamba msimamo wake na mtazamo wake wa kuichukulia Korea Kaskazini kama taifa linaloikinga dhidi ya uwepo wa Marekani umebadilika.
Beijing inahofia kwamba iwapo serikali ya Korea Kaskazini itasambaratika, basi maafisa wa usalama wa Marekani wataingia humo na kuweza kufikia mpaka wa China.
Na ingawa Korea Kaskazini inaendelea kuisumbua China, Marekani kiasi ni adui mkubwa zaidi kwa China ukitazama upande wa maslahi ya mataifa hayo mawili.
Ahadi ya Tillerson majuzi kwamba Marekani haitaki kubadilisha uongozi wa Korea Kaskazini ilionekana sana kulenga kuishawishi China badala ya Pyongyang.
Kutotabirika: Hata anaposhughulikia taifa kama Korea Kaskazini, Rais Trump hutaka sana kutotabirika. Na mbinu zake huwa ni za watu wa kufanikisha makubaliano ya kibiashara ya kuwafaa binafsi.
Hata hivyo, wachanganuzi wanatatizika kufasiri tofauti zilizojitokeza kati ya msimamo wake mkali awali na tamko lake la karibuni kwamba anaweza kufurahia kukutana na Kim Jong Un - mazingira yakiwa mahususi.
Barack Obama pia alisema wakati wa kampeni za urais mwaka 2008 kwamba angelipenda kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini.
Lakini hakumsifu kiongozi huyo kama alivyofanya Trump majuzi, aliposema Kim ni kijana mwerevu bila shaka kwani aliweza kudhibiti madaraka baada ya kifo cha babake licha ya kwamba alikuwa na umri mdogo.
Haijabainika iwapo Trump alikuwa anatoa maneno hayo kama chambo, au alikuwa kweli anataka kukutana na Kim Jong Un au alikuwa tu anatoa tamko hilo kuwachezea watu akili.
Kutotabirika: Hata anaposhughulikia taifa kama Korea Kaskazini, Rais Trump hutaka sana kutotabirika. Na mbinu zake huwa ni za watu wa kufanikisha makubaliano ya kibiashara ya kuwafaa binafsi.
Hata hivyo, wachanganuzi wanatatizika kufasiri tofauti zilizojitokeza kati ya msimamo wake mkali awali na tamko lake la karibuni kwamba anaweza kufurahia kukutana na Kim Jong Un - mazingira yakiwa mahususi.
Barack Obama pia alisema wakati wa kampeni za urais mwaka 2008 kwamba angelipenda kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini.
Lakini hakumsifu kiongozi huyo kama alivyofanya Trump majuzi, aliposema Kim ni kijana mwerevu bila shaka kwani aliweza kudhibiti madaraka baada ya kifo cha babake licha ya kwamba alikuwa na umri mdogo.
Haijabainika iwapo Trump alikuwa anatoa maneno hayo kama chambo, au alikuwa kweli anataka kukutana na Kim Jong Un au alikuwa tu anatoa tamko hilo kuwachezea watu akili.
Tupia Comments: