Serikali kupitia Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dr. Mbarawa, imesema sio kweli kwamba ndege iliyonunuliwa na serikali ni miongoni mwa ndege ya terrible teens ambazo zimekosa soka, kutokana na kuwa na uzito mkubwa unasababisha kula mafuta zaidi na haziwezi kwenda umbal mrefu bila kuongeza mafuta.
Terrible teen ni ndege za mwanzo Aina ya dreamliner 787 zilizotengenezwa na miaka 6-7 iliyopita. Ndege iliyonunuliwa ina uzito kidogo ukilinganisha na dreamliner za zamani, za sasa 787 zina uzito wa tani 4-6 ukilinganisha na dreamliner za mwanzo
Kati ya ndege hizo Terrible teen zilizokosa soka , Terrible namba 13 n 14, 16, 17, 18 ethiopia airways wameonyesha nia ya kuzichukua, terrible teens line namba 11 inatumiwa na boeing business jet, namba 12 Ethiopia airways wameonyesha nia kuichukua, terrible teens line namba 4 na namba 5 zinatumiwa na boeing kama testing aircraft
Ndege inayoonyweshwa kwenye mitandao line number yake ni 19 na ya kwetu ni line namba yake ni 719, Napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu kuwa Serikali imenunua ndege mpya na ya kisasa na kwa bei nafuu dreamliner inatumia injini za aina 2 ya RR au GE, ndege tuliyonunua sasa hivi inajengwa na kinachoendelea sasa hivi tunachagua engine kabla ya ndege kumalizwa unapewa uhuru wa kuchagua engine. Serikali imeweka ratiba ya kufuatilia ndege hiyo hatua kwa hatua mpaka ikamilike
Tupia Comments: