Mgogoro uliopo ndani ya Cuf ni mkubwa sana.
Maalim Seif unaushawishi mkubwa ndani ya Cuf, pia fahamu kwamba Lipumba nae anaushawishi mkubwa tu kama ulivyo wewe.
Habari ya mashabiki ndani ya mitandao ya kijamii si suluhu ya kumaliza mgogoro huu.
Umesikika ukisema ni Bora uzungumze na CCM, lakini si Lipumba. Mimi nasema hapana.
Mgogoro huu Utamalizwa kwa wewe na Lipumba kukaa mezani na kujadiliana Nini kifanyike ili muendelee na ujenzi wa Chama chenu.
Shirikisheni wanataaluma mbalimbali wa masuala ya kisiasa, kisheria, kijamii na kitamaduni katika maridhiano yenu.
Wapambe walio nyuma yenu si wema hata kidogo.
Msipo kubali kukaa na kuyamaliza kwa majadiliano hakika hata patikana mshindi. Matokeo yake mnaiua CUF kwa mikono yenu wenyewe.
Mmeijenga kwa jasho na Damu nyingi za wanachama wenu lakini haya hamkumbuki hata kidogo kwa kua kuna misukumo nyuma yenu isio salama.
Namalizia kwa kusema kwamba mchawi wa CUF ni wewe Maalim Seif na Lipumba.
Mtasingizia kila kundi, kila Raia.
Kubalini kukaa mezani na kuyamaliza.
Tupia Comments: