Mbunge wa jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam, Abdalah Mtolea amesema kuwa hakubaliani na zuio la kukataza barua yake ya kuomba wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) kuzuiwa kufanya usafi wa mazingira katika ofisi ya chama hicho zilizopo Buguruni jijini hapa, kazi iliyotarajiwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu.
Akaongeza kuwa tangu Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamishna Simon Sirro juu ya kuzuiwa kwa shughuli hiyo, Mtolea amekuwa akimtafuta Kamishna Sirro lakini hapokei simu zake na hata alipomfuata ofisini kwake, Jumamosi, alishindwa kuonana naye.
Akizungumza na mtandao huu, mbunge huyo alisema anamtafuta Kamanda Sirro kwa ajili ya kupewa ufafanuzi wa zuio la shughuli yao ya kufanya usafi lakini mawasiliano yamekuwa magumu, hivyo ameamua kumuandikia barua.
“Namwandikia barua Kamishna Sirro ili ndani ya wiki mbili Ofisi ya Chama Cha Wananchi (CUF) ikafungwe maana sisi tulihitaji tukaifanyie usafi lakini wametuzuia bila maelezo ya kujitosheleza hivyo namwomba Kamishna Sirro ndani ya muda wa wiki mbili akaifunge ofisi hiyo kutokana na baadhi ya vikundi kuifanya kama nyumba ya kujifunzia kareti na kutumia kwa manufaa yao binafsi,” alisema.
Kamishna wa Polisi Kanda MaalumDar es Saalaam, Simon Sirro akizungumza na wanahabari ofisini kwake, April 28, 2017 (Ijumaa), alisema kuwa sababu ya kupiga marufuku barua hiyo ya mbunge ni kutokana na sababu za kiusalama pamoja na mgogoro wa muda mrefu unaoendelea ndani ya chama hicho.
Akashauri badala yake kila mwanachama wa CUF au mwananchi afanye usafi katika eneo lake analoishi au ofisi yake anayofanyia kazi na kwamba kitendo hicho cha wanachama hao kukusanyika kutoka maeneo mbalimbali kwa kigezo cha kufanya usafi kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Tupia Comments: