MKOA wa Arusha Umeendelea Kukumbwa na baa la Ajali ,ambapo ikiwa haijakatika hata wiki toka ajali ya basi la shule kuua wanafunzi 36,leo hii kumetokea ajali nyingine ya nyumba kuangushwa na mti uliokuwa unasombwa na maji mengi,hali iliyopelekea vifo vya watu 5 na wawili kujeruhiwa.
Taarifa zilizotufiki hivi punde kutoka Jijini Arusha ,Zinasema kuwa mti huo uliseleleshwa na maji kwa umbali wa mita mia kabla ya kufikia nyumba hiyo na kusababisha watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo kupata ajali hiyo.
Taarifa zaidi ziwawajia kadri tutakavyozipokea kutoka Jijini Arusha.
Tupia Comments: