Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Godbless Lema ametoa masikitiko yake na kuonyesha kuumizwa na kitendo alichofanyiwa jana wakati wa kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva waliofariki katika ajali ya basi.
Lema anasema kitendo cha yeye kama Mbunge wa Arusha mjini pamoja na Meya wa jiji kunyimwa nafasi japo ya kutoa pole kwa familia na wafiwa wakati wa kuaga miili hiyo ni ubaguzi mkubwa.
==>Huu ni Ujumbe wa Godbless Lema
Leo(jana) katika msiba wa kuaga Wanafunzi waliofariki ktk ajali . Mimi kama Mbunge mwenyeji niliyefiwa Jimboni kwangu pamoja na Mayor tulihudhuria maombolezo hayo, ilikuwa ni itifaki ya kawaida kabisa kuelewa kuwa Mbunge pamoja na Mayor watapaswa kutoa salamu za rambi rambi au kuwashukuru wageni waliofika kwa ajili ya kutupa pole .
Nilisikia toka jana jioni kuwa katika maombolezo haya leo kuwa Viongozi wa Chadema watapaswa kutokuongea , nilimpigia simu Mbunge wa Ngorongoro Mh Ole Nasha , nikamweleza ubaguzi mchafu unavyopangwa katika jambo hili muhimu la kuaga watoto wetu, alinihakikishia kuwa Makamu wa Rais asingeweza kukubaliana na ujinga huu.
Kwenye ratiba nilipoingia uwanjani , jina langu lilikuwepo kwenye ratiba kwa ajili ya salamu za rambirambi, lakini baada ya Mkuu wa Mkoa kukabidhiwa itifaki, mambo yalibadilika na ilionekana dhahiri kuwa sitakiwi kabisa kutoa pole kwa watu wa jimbo langu waliofikwa na msiba huu mbaya. M/kiti Mbowe aliandika meseji kwenda kwa M/ Rais kukumbusha umuhimu wa wenyeji kutoa salamu , Makamu wa Rais baada ya kupokea meseji hiyo, alimwita Mkuu wa Mkoa , ndipo ilionekana kama kuna ushindani unatokea kati yao , lakini hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kutoa salamu kwa wapendwa wetu.
Wabunge wa CCM waliokuwepo ambao ni mawaziri wote waliweza kutoa pole ,huu ni ubaguzi uliojaa ujinga na chuki mbaya kisiasa, nitaeleza madhara yake kwenye hotuba yangu kesho , lakini nafikiri watoto mara nyingi huwa wanafuata walichofundishwa na wazazi , pengine ingekuwa ni usaliti Mbunge Lema kusalimia na kuwapa pole watu wake mbele ya Makamu wa Rais. Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama nchi na Syria ni wakati.
Nawashukuru wote waliotukimbilia kwa matatizo yaliyotokea Arusha, Mungu awabariki sana. Msiogope , Mungu hadhiakiwi apandacho mtu ndicho avunacho
Tupia Comments: