Wimbi la ajali limezidi kujitokeza nchini Tanzania ambapo leo Jumanne May 9,2017 basi la Ally's kutoka Mwanza kwenda Kaliua Tabora limegongana uso kwa uso na basi la Isanzu lililokuwa likitoka Kahama kwenda Mwanza.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa mbili asubuhi katika eneo la Samuye barabara ya Shinyanga kwenda Mwanza ambapo inaelezwa kuwa dereva wa basi la Izanzu hai yake ni mbaya.
Hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini watu kadhaa wamejeruhiwa na wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mabasi yakiwa yamegongana
Majeruhi wakipatiwa matibabu hospitali ya mkoa wa Shinyanga
Tupia Comments: