Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza muhtasari wa muelekeo wa bajeti kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 kwa mara ya kwanza kufikia Shilling Trilion 1,081.4 ambapo ikitengemea makusanyo ya kodi ya ndani ya nchi.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Waziri wa Fedha na Mipango Dr.Khalid Salum Mohamed amesema muelekeo wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa Fedha utatengemea vyanzo vyake vya ndani vya mapato vinavyokusanywa na taasisi za kodi nchini,mamlaka ya kodi TRA pamoja na bodi ya mapato ZRB.
Amesema taasisi hizo ambapo TRA inatarajiwa kukusanya jumla ya shilling Billion 258.7 wakati bodi ya mapato ZRB inatarajiwa kukusanya Shilling Billion 347.3 kwa mwaka.
Alifahamisha kuwa hii ni mara ya kwanza kwa bajeti ya serikali kufika katika kiwango hicho cha Fedha ambapo miaka 2016-2017 ilifika Shilling Billion 841.5 kwa mwaka ambapo bajeti ya mwaka huu haitatengemea Fedha za wahisani na washirika wa maendeleo.
Mapema dk.Salum amevitaja vipaumbele vya serikali ni pamoja na kuimarisha huduma za kijamii ikiwemo afya,elimu pamoja na miundo mbinu ya ujenzi wa barabara hadi vijijini.
Hata hivyo amesema miradi ya ujenzi wa miundo mbinu imepewa kipaumbele katika kuingiza mapato ikiwemo kukamilika kwa jengo la abiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume,Bandari mpya ya mpiga duri huko Maruhubi
Tupia Comments: