Mara nyingi watanzania wamekuwa wanataja mafanikio ya nchi nyingine wakilinganisha na mazingira hafifu ya hapa nchini katika masuala ya Maendeleo.
Lakini orodha ya mazuri yanayoigwa na nchi nyingine kutoka Tanzania itakuwa imeongezeka kwa jambo moja lingine ambalo ni Mabasi ya mwendo kasi.
Aidha, Mamlaka ya usafiri jiji la Nairobi imefufua mpango kupunguza foleni za magari kwa kuanzisha usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi kama yanayotumika kwa sasa nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Katibu wa Masuala ya usafirishaji Mwangi Mariga alisema ujenzi wa mradi huo wa Mabasi ya Mwendokasi utahusisha miji mitano.
Naye Katibu wa Baraza la Mawaziri James Macharia alishauri mwaka jana kwamba mapendekezo maalum ya mfumo wa Mabasi ya usafiri yalikuwa na changamoto kutokana na miundombinu iliyopo ya barabara kwa mabasi kuwa na msongamano.
Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi umebuniwa kufuatia idadi ya watu wa Nairobi kuongezeka hadi milioni 3.3 kutoka 350,000 mwaka 1963 na idadi ya magari inakadiriwa kufikia 300,000 bila ongezeko sawa katika mtandao wa barabara.
Tupia Comments: