Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanza kumfanyia uchunguzi Mzee Francis Maige Kanyasu ambae ni mchoraji wa Nembo ya Taifa ya Tanzania.
Dk. Juma Mfinanga amesema ambae ni mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali amesema Mzee huyo amechukuliwa leo asubuhi kutoka Hospitali ya Amana ambako alipelekwa jana na majirani zake na kupatiwa matibabu ya awali.
‘’ Tumemchukua kutoka Hospitali ya Amana baada ya kupata habari zake kwenye vyombo vya habari kuwa hali yake kiafya sio nzuri hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa MNH , Profesa Lawrence Museru akatuagiza tumfuate ili apatiwe matibabu hapa Muhimbili ‘’ Amesema Dk. Juma.
‘’ Wenzetu wa Hospitali ya Amana wamemfanyia uchunguzi wa awali na wakatueleza shida yake kubwa ni kukosa nguvu na kushindwa kutembea hivyo tumemleta hapa Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Baada ya uchunguzi tutamuanzishia tiba haraka kwa kushirikiana na Idara zingine hapahapa MNH.’’ Amesema Dk. Juma.
Kwa mujibu wa Dk. Juma kukosa lishe , mazingira magumu pamoja na umri kunasababisha mtu kupata magonjwa mbalimbali.
Tupia Comments: