Watu 80 wameuawa na wengine zaidi ya mia tatu kujeruhiwa, baada ya bomu lililotegwa kwenye gari kuripuka mjini Kabul.
Maafisa nchini humo wanasema mlipuko mkubwa ambao umetokea katika eneo la makazi ya wanadiplomasia mapema asubuhi.
Aidha nyumba zilizokuwa jirani na bomu hilo lilipolipuka pia zilipatwa na madhara kwa madirisha na milango kupasuka.
Tupia Comments: