Wizara ya nchi ofisi ya raisi Katiba , Sheria ,Umishi wa Uma na utawala a Bora imesisitizwa kuangalia kwa kina suala la nafasi ndogo za uajiri wanazopewa Watu wenye ulemavu katika taasisi za serikali ili waweze kujumuika katika shughuli za kuleta maendeleo Nchini.
Akichangia  hutuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2017 -2018 ya wizara hiyo mwakilishi wa nafsi za wanawake kupitia watu wenye ulemavu Zainab Adallah amesema mbali na osifi ya utumishi kuwa mstari wa mbele kutangaza nafasi za ajira kwa wananchi lakini wanashindwa kuweka nafasi maalumu za watu wenye ulemavu jambo ambalo linawakosesha haki zao za msingi.
Hata hivyo amesema pindipo watu wenye ulemavu watapewa fursa za ajira katika sekta za Serikali na watu binafsi ,zitawasaidia kuweza kujikimu katika familia pamoja na kuondokana na utegemezi katika jamii.
Aidha wamesema jamii inayoishi na watu wenye ulemavu Imekuwa na Mwamko mkubwa katika kuwapeleka watoto wao kujifunza masomo ya skuli na fani mbalimbali za ujasiriamali lakini wanashindwa kufikia malengo kutokna na kukosa fursa za ajira kwa waajiri.

Tupia Comments: