Mtu mmoja ameuawa na wengine 19 kujeruhiwa wakati gari liliendeshwa kuenda sehemu ya kupitia watu eneo la Times Square mjini New York, Marekani.
Dereva wa gari hilo amekamatwa na eneo hilo kufungwa kwa mujibu wa idara ya polisi ya mji wa New York.
Gari hilo linaripotiwa kuruka vizuizi kwenye mtaa wa 45 katika eneo maarufu la watalii.

 Picha zilionyesha gari nyekundu aina ya Honda likiwa limepinduka huku likifuja moshi

Dereva wa gari hilo mwenye umri wa miaka 26 anafanyiwa uchunguzi wa pombe.

Anaripotiwa kuwa na historia ya kuendesha gari akiwa mlevi.
Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakiondolewa eneo hilo.

Polisi wanasema kuwa dereva alipoteza mwelekeo na huenda kisa hicho kinaonekana kuwa ajali.
Waliongeza kuwa kisa hicho hakina uhusiano na ugaidi.

Tupia Comments: