Kamati ya amani ya kitaifa ya viongozi wa dini Zanzibar imewataka viongozi nchini kuendelea kushirikiana na mkuu wa mkoa wa mjini magharib Ayob Mohd Mahmoud katika jitihada za kukemea vitendo viovu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati hiyo Sheikh Salim Mohd Hassan huko katika ukumbi wa mazson hotel amesema kufanya hivyo kutasaidia kurejesha maadili ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa yameonekana kuporomoka.
Amesema kuwa mkuu wa mkoa ameweza kuondosha baadhi ya nyumba ambazi zimekuwa zikitumika kufanyia vitendo viovu pamoja na kupiga vita utumuaji na uingizwaji wa dawa za kulevya .
Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa katika sehemu husika mara vinapoibuka vitendo viovu katika maeneo yao ili kuthibiti kuongezeka kwa vitendo hivyo ambavyo vinaweza kusababisha kupotea kwa amani ya nchi.
Nae katibu wa mufti mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhili Sulleiman Suraga amewasisistiza jamii kuacha kufanya vitendon viovu hasa katika kipindi hichi cha kuelekea mwezi mtukufu wa ramadhan.
Kikao hicho kimeandaliwa kufuatia kauli za  baadhi ya viongozi kutokuwa pamoja na mkuu wa mkoa wa mjini magharib kupinga vitendo viovu.

Tupia Comments: