Korea Kaskazini imesema kuwa itafanya mazungumzo na Marekani iwapo mazigira yataruhusu ,kulingana na vyombo vya habari vya Korea Kusini.
Mjumbe mwandamizi wa Korea Kaskazini amesema kuwa mazungumzo na serikali ya rais Trump yanawezekana kufuatia mkutano na waliokuwa maafisa wa serikali ya Marekani nchini Norway.
Awali mwezi huu rais wa Marekani Donald Trump alisema itakuwa heshima kubwa kukutana na rais Kim Jong un.
- Trump: tutaidhibiti Korea Kaskazini
- Trump asema Korea Kaskazini ni tatizo
- Trump aionya tena Korea Kaskazini
Matamshi yake yanajiri kufuatia ongezeko la hali ya wasiwasi kuhusu mipango ya Korea Kaskazini ya kinyuklia pamoja na ile ya utengezaji wa makombora ya masafa marefu.
Choe Son Hui ambaye ni afisa katika wizara ya maswala ya kigeni kuhusu maswala ya Marekani kaskazini alitoa matamshi hayo wakati alipokuwa akirudi Pyongyang baada ya mkutano mjini Oslo.
Tupia Comments: