Rais Trump na aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la FBI nchini Marekani James Comey
Ikulu ya Whitehouse nchini Marekani imekana ripoti kwamba rais Donald Trump alimfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi FBI James Comey kwa kukataa kumtii
Katibu wa maswala ya habari Sean Spicer alikana habari za vyombo vya habari kwamba rais alimtaka bwana Comey kufanya hivyo katika mkutano wa faragha ndani ya Ikulu ya Whitehouse mnamo mwezi Januari.
Kulingana na gazeti la New York Times, bwana Comey alisema kuwa yuko tayari kuwa mwaminifu lakini sio kumtii kwa rais.
Rais Trump amekumbwa na pingamizi chungu nzima kwa kumfuta bwana Comey siku ya Jumanne .
Uchunguzi wa FBI kuhusu hatua ya Urusi kuingilia siasa za Marekani na iwapo maafisa wa Trump walishirikiana na taifa hilo, zimekumba uongozi wake wa kipindi cha muda mchache.
Katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Ijumaa, bwana Spicer alikataa kuzungumzia kuhusu maswala ya iwapo bwana Trump amekuwa akirekodi mikutano yake.
Bwana Trump alituma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba bwana Comey ''atumai kwamba mazungumzo yao hayakurekodiwa''.
Bwana Spicer alikana madai kwamba chapisho hilo la bwana Trump lilikuwa la vitisho.
''Rais hana jingine la kuongezea'',aliwaambia maripota wakati aliposhinikizwa kuzungumza.
''Chapisho hilo linajieleza''.

Tupia Comments: