Timu ya Manchester United ambao pia ni mabingwa wa kombe la Europa League, wametangaza jezi ambazo watakuwa wakizivaa katika mechi zao za nyumbani katika msimu ujao wa 2017/18.
Jezi hizoambazo zinatengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas, zinafanana na zile walizozitumia katika msimu uliopita lakini hizi mpya zimeongezwa kwa kuwekewa rangi nyeusi mikononi.
Timu hiyo inatarajia kuanza kucheza mechi zake za maandalizi kuanzia Julai 15 ya mwaka huu nchini Marekani, ambapo wataanza kwa kuchuana na LA Galaxy ya nchini humo. United inatarajiwa kucheza mechi saba katika maandalizi hayo, ambazo ni pamoja na Barcelona, Manchester City, Real Madrid, Sampdoria na nyingine.


Tupia Comments: