Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi imetoa onyo kali kwa wanaochimba mchanga ovyo ambao huikosesha mapato serikali kwa kutofuata sheria na taratibu za nchi zilizowekwa.
Hayo yameelezwa huko WAWI katika Ukumbi wa Makonyo Chake Chake Kisiwani Pemba na Waziri wa Wizara hiyo HAMAD RASHID MOHAMMED Wakati akizungumza na wafanya kazi na wachimbaji wa mchanga.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haizuii uchimbaji huo bali wanacho kizuia ni kuwepo kwa baadhi ya watendaji hao kuzikiuka na kutozifuata Sheria na taratibu zilizopo.
Hata hivyo amesema Wizara yake itahakikisha kwamba Sheria na taratibu hizo zinafuatwa huku akizitaja Ada elekezi ambazo zimewekwa na Wizara hiyo zina paswa kufuatwa na wafanya kazi hao ili kuondosha ulaghai unao weza kufanywa na baadhi ya watendaji hao huku akikanusha vikali kuuzwa kwa mchanga Kisiwani Pemba.
Ameeleza kuwa Wizara yake itaweka Ulinzi maalum katika Sehemu za Uchimbaji kwani imebainika kwamba baadhi ya Madereva wasiokua waaminifu huenda usiku na kuchimba mchanga huo kinyemela.
Kuwepo kwa maeneo yakutosha katika uendeshaji wa shughuli hizo hapa Kisiwani Pemba Serikali imeruhusu Uchimbaji mchanga kufanyika kutokana na kuwepo kwa wingi wa Rasili mali hiyo, miongoni mwa Sehemu hizo ni WAWI,KISHINDENI na UWAANI Kwa lengo la kuipatia mapato nchi ya Zanzibar.
Tupia Comments: