Baada ya ukimya wa muda mrefu sana wa mkongwe wa muziki wa Bongofleva Ferooz Mrisho 'Ferooz' siku za hivi karibuni ametajwa kuwa ni miongoni mwa wasanii wanaotumia madawa ya kulevya na ndiyo sababu iliyompoteza kwenye ramani ya muziki.
Baada ya madai ya majirani zake kuwa Ferooz anavuta bangi na kutumia madawa ya kulevya kitu kinachompelekea ashindwe kuendelea na muziki.“Ni mara kumi upate UKIMWI kuliko uwe unatumia madawa ya kulevya, nawashauri watu wengine pamoja na wasanii wenzangu wasije wakajaribu kufanya hivyo, kwani misongo ya mawazo ndo huwa inawapelekea wasanii kuingia katika matumizi hayo ya madawa ya kulevya ”.
Alisema FerooZ Ameongezea kwa kusema kuwa amekuwa akitafuta sapoti kwa mastaa wanaotikisa kwenye bongofleva kwa sasa lakini wemekuwa wakimpangusa 'Kumpotezea'.

Tupia Comments: