Idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao kutokana na mzozo ndani ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo mwaka uliopita, ilikuwa ni ya juu kuliko idadi ya watu waliohama makwao nchini Syia na Iraq.
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ilishuhudia ongezeko la watu 922,000 waliohama kutokana na mzozo mwaka uliopita, ikilinganishwa na watu 824,000 waliohama nchini Syria na 659,000 nchini Iraq.
- Waasi wa M23 waingia DRu
- Maafisa wa UN waliotekwa DRC waachiliwa huru
- Mhubiri kutoka DRC apewa hifadhi Afrika Kusin
- Badibanga atangazwa kuwa waziri mkuu DRC
Watafiti kutoka baraza ya wakimbizi nchini Norway NRC walihesabu zaidi ya watu 922,000 ambao walilazimika kukimbia makwao ndani mwa DRC mwaka 2016.
Katibu mkuu wa NRC Jan Egeland aliiambia BBC kuwa ni jambo la kushangaza kuwa sio Syria au Iraq zilizo na wahamiaji wengi.
Tupia Comments: