Polisi nchini Indonesia waliwakamata wanaume 141 ambao walikuwa wanahudhuria sherehe ya wapenzi wa jinsia moja katika mji mkuu wa Jakarta, siku ya Jumapili.
Polisi wanasema kila aliyehudhuria, akiwemo raia mmoja wa Uingereza na mwingine wa Singapore walilipa kiingilio cha rupia elfu 185 (Dola 14; Pauni 10).
Indonesia imeshuhudia kuongezeka kwa chuki kwa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Mapenzi kati ya watu wa jinsia moja sio marufuku kulingana na sheria za Indonesia, isipokuwa katika mkoa wa kihafidhina wa Aceh.
Lakini msemaji wa polisi wa Jakarta Raden Argo Yuwono alisema baadhi ya wale walio kizuizini wanaweza kushtakiwa chini ya sheria kali ya Indonesia ya kupambana na vitendo vichafu.
"Baadhi yao walipatikana wakiwa wamevua nguo na wakishiriki ngono na wengine kujipiga punyeto wakati wa tukio," aliiambia BBC Indonesia.
Chini ya sheria hizo kali za Indonesia, kuandaa onyesho kama hili ili kuwatumbuiza watu inaweza kufasiriwa kama kosa la kutenda kitendo kichafu eneo la umma.
Wiki iliyopita, wanaume wawili walihukumiwa kuchapwa viboko mbele ya umma katika mkoa wa Aceh, baada ya kupatikana wakifanya ngono.
Sheria kali dhidi ya uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja zilianza kutekelezwa nchini humo mwaka wa 2014.
Mapema mwezi huu, polisi huko Indonesia waliwatia mbaroni watu 14 katika mji wa Surabaya.
Tupia Comments: