Kivuko cha MV KAZI kwa mara ya kwanza kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari baada ya kukamilika kwa matengenezo yake.
Majaribio hayo yalifanyika kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini ambayo inavitaka vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness Certificate”.
Mkuu wa Vivuko Magogoni/Kigamboni, Mhandisi Lukombe King’ombe  alisifu uwezo wa kivuko hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho kwani kitawasaidia kupunguza msongamano wa abiria na magari hasa majira ya asubuhi na jioni.
Ujenzi wa MV KAZI ambacho kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170. umegharimu jumla ya Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania.

Tupia Comments: