Serikali mpya imeapishwa siku ya Ijumaa baada ya majadiliano ya muda mrefu ya rais Omer Al Bashir nchini Sudan.

Kwa mujibu wa habari,wabunge 31 wameapishwa katika ikulu mbele ya rais Omer huku rais huyo akitaka kila mmoja wao kuwa muadilifu na kusaidia kuleta amani nchini humo.

Rais Omer amesema jambo kama hilo halijawahi kutokea nchini humo na uamuzihuo wa kuapisha serikali hiyo ni kutokana na shinikizo la vyama vingi.

Serikali ya Sudan imeundwa na kuapishwa mbele ya jeshi la nchi hiyo na vyama tofauti.

Hata hivyo baadhi ya vyama vilikataa kuhudhuria hafla hiyo na kusema kuwa hiyo ni ishara ya rais Bashir kuwa na mamlaka makubwa kupita kiasi.

Tupia Comments: