Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amefikishwa Hospitali  ya Taifa Muhimbili (MNH) leo akitokea Dodoma kwa ajili ya matibabu ya uvimbe unaomsumbua.

Mdogo wa mbunge huyo, Edward Heche amesema kuwa kaka yake alianza kupatwa na maumivu makali jana (Jumatano) akiwa Dodoma ndipo alipokwenda kwa ajili ya kumsaidia.

 “Nilifika Dodoma jana saa tisa nikamkuta anatibiwa katika hospitali ya Bunge hali yake haikuwa nzuri alikuwa analalamika kuwa maumivu yalizidi, tukampelekea hospitali ya mkoa bado aliendelea kulalama huko akapewa dawa za kupunguza maumivu lakini haikusaidia tulipoandikiwa kuja Muhimbili,” amesema na kuongeza;

“Hali ya Heche sio nzuri, tatizo ni kwamba alifanyiwa upasuaji kwenye uvimbe uliokuwa pajani lakini kwa bahati mbaya inaonekana baadhi ya nyuzi ziliachia na ndiyo inamsababishia maumivu makali.”

Tupia Comments: