Shirika la umeme Tanzania-Tanesco limeanza oparesheni ya kukata umeme kwa wadaiwa sugu wenye madeni makubwa ambapo leo makampuni makubwa mawili yamekumbwa na zoezi hilo ikiwemo kiwanda cha uchapaji cha I Print barabara ya Nyerere banda la ngozi na Fida Hussein kilichopo vingunguti jijini Dar es salaam.

Zoezi hili ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la kuwakatia umeme wale wote wanaodaiwa bila kujali taasisi za serikali wala binafsi ambapo makampuni haya yote mawili yanadaiwa kiasi cha shilingi milioni 45.

Awali akizungumza na waandishi wa habari meneja Tanesco mkoa wa Ilala Mhandisi Athanasius Nangali amebainisha kuwa mkoa wake ulikuwa unadai kiasi cha shilingi bilion 7, bilion 6 kati yake ni taasisi za seriksli na bilion 1 sekta binafsi ambazo hata hivyo tayari zimelipwa kwa asilimia 90 huku serikali ikiwa imelipa bilionI 2 tu ingawa imeonyesha ushirikiano kwa kuingia mkataba wa kulipa deni lililobaki.

Zoezi hilo litakuwa ni endelevu kwani limelenga kukusanya madeni yote kwa wadaiwa sugu ikowemo wa serikali na sekta binafsi.

Tupia Comments: