Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kubakia na mumewe baada ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais wa Nigeria.
Garba Shehu aliambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.
Wasichana 82 waliachiliwa huru ikiwa ni kati ya mazungumzo yalioafikiwa na shirika la ICRC.
Serikali ilikubali kuwaachilia huru wanachama wanne wa Boko haram kubadilishana na uhuru wa wasichana hao duru ziliambia BBC.
Wapganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasich00 kana 1ati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.
Inaaminika kwamba baadhi ya wale waliotekwa wameolewa wapiganaji na wamepata watoto nao.
Tupia Comments: