WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani) ameagiza kuanzia sasa miradi yote ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) itumie nguzo na transfoma zinazotengenezwa nchini.
Alisema hayo juzi mjini hapa wakati akizindua Bodi ya Nishati Vijijini. Alisema ni vyema wakandarasi wa mradi huo wakafuatiliwa mahali wanaponunua vifaa. “Naagiza miradi yote ya REA awamu ya tatu itumie nguzo zinazozalishwa nchini, wakandarasi wote wanunue nguzo za Tanzania, zikiisha ndio waende nje ya nchi,” alisema.
Alisema tayari amepokea malalamiko kuwa nguzo zisizo na hadhi zinataka kununuliwa na kuna nguzo nyingine hazidumu hata miaka mitatu. “Hata transfoma tunataka zinazotoka ndani ya nchi, kuna kampuni Wanaosambaza chakula kibovu kushughulikiwa Muhongo azuia REA kutumia nguzo na transfoma za nje 202750005 ya Tanalec waelekezwe wafanye uzalishaji wa kutosha, transfoma nyingi za kutoka nje ya nchi zina matatizo,” alisema.
Pia alitaka kampuni zote za nje ambazo zitatekeleza mradi huo zifanye kazi na wakandarasi wadogo wa Tanzania. “Lazima wakandarasi wote wadogo wawe wa kampuni za kitanzania na kuna madai kampuni kubwa hazilipi wakandarasi wadogo na wakandarasi wadogo hawalipi vibarua,” alisema.
Alisema hali hiyo imekuwa ikifanya vijana wanaofanya kazi ya kuchimba mashimo ya kusimika nguzo katika maeneo ya vijijini kutolipwa. Waziri huyo aliitaka bodi hiyo kukaa na wakandarasi watakaotekeleza miradi ya awamu ya tatu ili kujiridhisha na kila mkandarasi na kampuni yake aeleze historia yake na hiyo kazi ataiwezaje. Alisema katika REA awamu ya pili wakandarasi wanane walishindwa kazi na kuangalia kama majina yao yameingia katika miradi ya REA awamu ya tatu.
“Bodi lazima ikae na wakandarasi watakaotekeleza miradi ya awamu ya tatu na kila mkandarasi mjue historia yake na kama hiyo kazi ataweza. REA awamu ya pili iliyoisha wakandarasi wanane walishindwa kazi na mpewe majina kama wamewekwa katika awamu ya tatu,” alisema. Waziri Muhongo alisema lazima bodi ikae na wakandarasi hao na kuwauliza na kuangalia uwezo wao na makampuni yao ili kujiridhisha.
“Lazima muangalie kama ana uwezo muone, ukubwa wa bajeti, vitendea kazi walivyonavyo na wataalam walionao ni lazima maofisa wa REA na wale wa Shirika la Umeme (Tanesco) wawepo,” alitaka ubora wa kazi uangaliwe.
“Wabunge walipita Njombe walitutukana sana walikuta zaidi ya transfoma 20 zilikuwa zimekufa jambo kama hili halipendezi,” alisema. Mkurugenzi Mkuu wa Rea, Gissima Nyamo-Hanga alisema hiyo ni bodi ya nne ambapo kila baada ya miaka mitatu bodi mpya imekuwa ikiteuliwa.


Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa James Mdoe aliwataja wajumbe wanane wa bodi hiyo ni Mwenyekiti wake Dk Gideon Kaunda, wajumbe ni Amina Hussein, Innocent Luoga,Michael Nyagogo, Stella Mandago, Stolastica Jullu, Happiness Mhina na Theobard Manumbe.

Tupia Comments: