Wachezaji wa Yanga wanatarajia kuondoka leo usiku nchini Algeria kurejea nyumbani.
Sasa wanatarajia kuondoka na ndege ya Emirates badala ya Turkish Airways na imeelezwa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), limelazimika kutoa mkopo kwa klabu hiyo ili kuwakomboa.
Wachezaji saba na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa walichelewa ndege jijini Algeria
na kulazimika kusubiri hadi Jumanne kesho ndiyo waondoke na kutua nchini kesho.
Mkwasa alisema wataomba msaada kwa MC Alger waliokwenda kucheza nao na kufungwa mabao 4-0
kwa kuwa hawakuwa na fedha za kutosha.
Lakini msaada huo wa TFF utawafanya warejee haraka nyumbani na si Jumatano tena
kama ambavyo ilikuwa ikitarajiwa.
Tupia Comments: