WAKATI Yanga wakiumiza vichwa vyao baada ya Simba kupewa pointi za Kagera Sugar, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara, ameibuka na kudai kuwa angefurahi kama mchezo wao wa kuhitimisha msimu huu wangekutana dhidi ya watani wao hao ili wawafunge mdomo.

Manara anaamini hatua ya Yanga kupinga wao kupeta pointi tatu baada ya Kagera kumtumia beki Mohamed Fakhi huku akiwa na kadi tatu za njano wakati wa mechi kati ya timu hizo ni ufuatiliaji wa mambo yasiyowahusu.

“Kwa kuwa kuna huu utata unaochagizwa na Ndala (Yanga), tunaomba nao mechi ya kumpata bingwa ipingiwe Kaunda na waamuzi walete wao ila sisi turuhusiwe kucheza wachezaji kumi tu,” alisema Manara.

Kamati ya Saa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wiki iliyopita ilitangaza kuipora Kagera Sugar ushindi wake wa mabao 2-1 na kuipa Simba baada ya kubaini Fakhi alicheza mechi kati ya timu hizo huku akiwa na kadi tatu za njano.

Hata hivyo, uamuzi huo umepingwa na Kagera Sugar pamoja na Yanga kwa madai kwamba hizo ni hila zenye lengo la kuinufaisha Simba ili iweze kufikia lengo lake ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Sakata hilo limesababisha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuingilia Kati na sasa inatarajia kukutana leo kujadili suala hilo.

Tupia Comments: