Yanga kuifuata Mouloudia Club Alger


TanzaniaHaki miliki ya picha
Image captionKikosi cha watoto wa Jangwani, Yanga
Yanga Fc inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam leo Alhamisi kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Mouloudia Club Alger Jumamosi Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers.
Mabingwa hao wa Tanzania wataendelea kumkosa kiungo wao Mzambia, Justin Zulu aliyeumia Aprili 1, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema kwamba wanamtarajia Zulu kuanza mazoezi na hayumo kabisa kwenye mipango ya mchezo wa marudiano dhidi ya MC Alger.Kuhusu orodha ya wachezaji watakaokwenda Algeria, Mkwasa alisema itajulikana baadaye .
Yanga iliyoshinda 1-0 katika mchezo wa kwanza Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, inahitaji kwenda kulazimisha sare tu ugenini ili kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya pili mfululizo mwaka huu.
Mwaka jana, Yanga pia ilicheza hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola ikitoka kutolewa na Al Ahly ya Misri katika Ligi ya Mabingwa.

Tupia Comments: