Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinafanyika leo April 26, 2017 mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, 1964 chini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalim Julius Nyerere na hayati Sheikh Abeid Karume.
1. Ni siku ambayo Tanganyika na Zanzibar ziliungana.
2. Ni siku ambayo Tanzania ilizaliwa.
3. Siku ambayo maadhimisho haya yanafanyikia makao makuu ya nchi Dodoma kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.
Mgeni rasmi ni rais wa Tanzania na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi ya Tanzania.
Fuatilia uzi huu kwa live updates.
Rais MAgufuli anaingia Uwanjani
Wananchi wote wanaimba wimbo wa taifa wakiongozwa na rais Magufuli. Huu ni uzalendo mkubwa sana kwa nchi yetu upendo na mshikamano daima.Amiri jeshi mkuu anakagua gwaride.
Gwaride linaendelea kufanya vitu vyake sasa. Linalita kwa mwendo wa haraka mbele ya rais na mbele ya wananchi wote.
Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni;
Miaka 53 ya Muungano; Tuulinde na Kuuimarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii,”
======
Rais Magufuli: Siku ya leo ni siku ya pekee, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha hapa”
Rais Magufuli: “Siku ya leo ndiyo birthday ya Tanzania”
Rais Magufuli: ”Baadhi ya mambo yaliyowezesha kuanzishwa umoja wetu ni undugu hata kabla ya kuja wakoloni walikuwa wakishirikiana ikiwepo biashara”
Rais Magufuli: ”Ushirikiano mzuri uliokuwepo kwa vyama vetu vya ukombozi, viongozi na wanachama wa vyama hivi viwili walikuwa wakishirikiana”
Rais Magufuli: “Muungano wetu umewezesha kuwepo na uhuru, amani na umoja wetu”
Rais Magufuli: “Tumejenga miradi mbalimbali ya huduma za jamii, Tanzania ya sasa sio ile ya 1964”
Rais Magufuli: “Wahenga walisema usione vyaelea vimeundwa, wapo watu wamewezesha mafanikio haya kupatikana”
Rais Magufuli: “Swala la kulinda Muungano sio jambo rahisi hivyo hatuna budi kuwapongeza waliowezesha kuwepo kwa Muungano wetu”
Rais Magufuli: “Bahati nzuri leo hapa tunae Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume, tunawashukuru sana”
Rais Magufuli: "Napenda kuwaahidi mimi na Dk. Shein tutafata nyayo zenu za kudumisha Muungano"
Rais Magufuli: "Tukiwa tunaadhimisha miaka 53 ya Muungano tutafakari tulipotoka, tulipo sasa na tunapoenda, wengi wetu wamezaliwa baada ya mwaka 1964"
Rais Magufuli: "Kwa pamoja tunaweza, tukishikamana kwa pamoja tunaweza, na ninahakika kwa nguvu za Mwenyezi Mungu tutaendelea kusherehekea Muungano"
Rais Magufuli: "Pamoja na mafanikio lakini pia kuna changamoto, kuna kamati ya kushughulikia mambo ya Muungano ikiongozwa na Makamu wa Rais"
Rais Magufuli: "Kila Mtanzania anatakiwa kulinda Muungano wetu na njia bora ni kuchapa kazi"
Rais Magufuli: "Kwa mara ya kwanza tumefanyia Dodoma na hii ni nia ya dhati ya serikali ya kuwa makao makuu yawe Dodoma na niwahakikishie sasa tupo Dodoma"
Rais Magufuli: "Serikali imetenga Bilioni 200 ya kujenga ofisi na majengo, tuna miradi mingi ya maendeleo kwa ajili ya Dodoma"
Rais Magufuli: "Kwa kumaliza natoa shukrani kwa kamati ya maandalizi watu ni wengi ndani na nje wamejaa hii kweli inaonyesha Ddm ni makao makuu ya nchi"
Rais Magufuli: "Napenda kupongeza ngoma, na hasa hawa watani zangu wanavyozungusha shingo, wanazungusha kweli shingo"
Rais Magufuli: "Tunaadhimisha miaka 53 tukitambua watangulizi kweli waliulinda Muungano wetu"
Rais Magufuli: "Kikwete siku hizi anaonekana kijana kuliko mimi, anapendeza"
Rais Magufuli: "Muungano ndiyo jembe letu, na kamwe asijitokeze mtu atakaye jaribu kuvunja Muungano wetu akija akitokea atavunjika yeye"
Rais Magufuli: "Niwatakie sikukuu njema, Mungu ibariki Tanzania, asanteni sana"
Tupia Comments: