China imetangaza kwamba imefanikiwa kuzindua manowari yake ya kwanza ya kujiundia yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita.
Meli hiyo ya kivita ina uzani wa tani 50,000.
Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya karibuni zaidi ya kujiimarisha kwa taifa hilo katika nguvu za jeshi lake la majini.
Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini.
Inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020.
Meli hiyo ya kivita ilizinduliwa Dalian
Meli hiyo baada ya kung'oa nanga Dalian
Meli pekee kubwa ya kubeba ndege inayomilikiwa na China ni meli ya Liaonong, ambayo ni meli ya enzi za muungano wa Usovieti iliyofanyiwa ukarabati.
China ilinunua meli hiyo kutoka kwa Ukraine.
eli ya kwanza ya kubeba ndege ya China kwa Liaoning ilinunuliwa kutoka Ukraine
Meli ya Liaoning ilipokuwa inakabidhiwa rasmi kwa jeshi la wanamaji la China Septemba 2012
Tupia Comments: