Wananchi wa kitongoji cha Mahiga, kata ya Mwakitolyo, halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wameiomba serikali kuingilia kati amri ya kuondolewa ndani ya siku saba katika eneo la wachimbaji wadogo la Mahiga ili kumpisha mwekezaji kampuni ya uchimbaji madini ya kichina Henan Afro-Asian Geo-Engineering iliyopewa lessen na serikali kuanza shughuli za uchimbaji madini aina ya Dhahabu.
Wananchi hawa ambao wanajishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya dhahabu katika kitongoji hicho cha mahiga, kijiji cha Mwakitolyo wanakutana hapa kujadili barua ya kuondolewa kwao iliyotolewa na ofisi ya Madini Kanda ya kati, Magharibi, Shinyanga kumpisha mwekezaji.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack, amewataka wachimbaji wadogo kutumia maeneo ya kijiji cha Nyaligongo na eneo la namba tano, yaliyotolewa na Rais John Magufuli kufanya shughuli zao. Ofisi ya Madini kanda ya kati, magharibi Shinyanga imetolea leseni kwa mwekezaji huyo.
Tupia Comments: