Rais wa Ufaransa Francois Hollande amewapatia uraia wa Ufaransa Waafrika 28 walioipigania Ufaransa wakati wa vita vya pili vya dunia pamoja na mizozo mengine.
Wakongwe hao wa vita walio na umri kati ya sabini na nane na tisini wanahudhudhiria hafla katika ikulu ya Elysee.
Ijapokuwa wanajeshi wengi wa Afrika walirudishwa nyumbani, takriban wapiganji 1000 wa zamani wanaishi nchini humo .
Naibu Meya wa mji wa Paris ambaye ni mjukuu wa raia wa Senegal aliyepigana katika vita vya pili vya dunia amekuwa akifanya kampeni ya wakongwe hao kupewa haki zaidi.
Tupia Comments: