Taifa la Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo limesitisha ushirikiano wa kijeshi na Ubelgiji baada ya Brussels kukosoa chaguo la waziri mkuu la rais Joseph Kabila.
Ubelgiji ilisema kuwa uteuzi wa Bruno Tshibala ulienda kinyume na makubaliano ya ugawanaji wa mamlaka ambapo Upinzani ndio uliofaa kumchagua kiongozi huyo kutoka kwa wanachama wake.
Bwana Kabila alimteua bwana Tshabala wiki iliopita baada ya upinzani kushindwa kukubaliana kuhusu mtu wa kumchagua kuchukua wadhfa huo.
- Bruno Tshibala ndiye waziri mkuu mpya DR Congo
- Serikali na upinzani kugawana mamlaka DR Congo
- Serikali na upinzani waafikiana DR Congo
Serikali mpya inalenga kuandaa uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu kufuatia hatua ya rais Kabila kukataa kung'atuka mamlakani baada ya muda wake wa kutawala kukamilika mwezi Disemba iliopita.
Tupia Comments: