Ethiopia imeondoa majeshi yake katika mji muhimu katikati mwa Somalia ,katika msururu wa hatua za hivi karibuni za taifa hilo kujiondoa nchini humo.
Dhusamareb sasa unadhibitiwa na wapiganji walio na msimamo wa kadri, wa Ahlu Sunna Waljama'a.
Kundi la Ahlu Sunna limekuwa likikabiliana na kundi la al-Shabab ambalo linadhibiti maeneo mengi ya Somalia.
Wachanganuzi wanasema Ethiopia inaondoa vikosi vyake kutokana na ukosefu wa uungwaji mkono na jamii ya kimataifa.
Al Shabab linamiliki miji mingi iliowachwa na vikosi hivyo vya Ethiopia.
Ethiopia huchangia vikosi vya Umoja wa Afrika lakini pia ina wanajeshi wengine nchini Somalia.

Tupia Comments: