ZAIDI ya Wakenya 1,400 wanaunga mkono ombi la kutaka kuidhinishwa kwa matumizi ya mmea wa bangi baada anayewasilisha hoja hiyo kuwawasilisha ombi lake mbele ya bunge la seneti.
Iwapo ombi hilo la mtafiti Gwada Ogot litaidhinishwa haitakuwa haramu kupanda ama hata kuuza bangi nchini Kenya.
Gwada Ogot anasema kwamba matumizi ya kiafya pamoja na utumizi wa mmea huo viwandani unaojulikana kwa jina la sayansi kama Cannabis sativa una faida nyingi.
Anasema kuwa matumizi ya mmea huo yataimarisha hali ya uchumi.
Sheria ya Kenya inapiga marufuku utumizi wowote wa bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.
Ogot anaomba bangi kuondolewa miongoni mwa orodha ya vitu haramu na kutaka sheria mpya kuanzishwa ili kuweka bodi simamizi ya utumizi wa mmea huo.
Tupia Comments: