Waungaji mkono wa rais Donald Trump wa Marekani, ambaye bado hajatimiza siku 100 madarakani, wamekusanya zaidi ya dola milioni 13 za kimarekani kwa ajili ya kampeni yake ya uchaguzi ujao katika robo ya kwanza ya mwaka huu. Ripoti ya tume ya uchaguzi ya Marekani inasema, fedha hizo zimekusanyika kupitia kamati tatu, na sehemu kubwa ya fedha zinatokana na mapato ya uuzaji wa bidhaa zinazohusiana na Trump kama vile nguo, kofia na kikombe kwenye sherehe ya kuapishwa kwake iliyofanyika mwezi Januari mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tupia Comments: