Kampuni Tanzu ya chakula na vinywaji nchini DMG Tanzania inakusudia kujenga kiwanda cha kusindika mchanganyiko kwa kahawa, maziwa na sukari na kuwa bidhaa moja itakayomrahisishia mtumiaji, tofauti na ilivyo sasa ambapo kila bidhaa inajitegemea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Rayton Kwembe ameeleza nia hiyo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa bidhaa hiyo iliyopewa jina la ‘Nuru Coffee Chap chap’ kwa ajili ya soko la Tanzania.
Amesema teknolojia ya uzalishaji huo inapatikana nchini Korea Kusini, na kwamba majadilaino ya awali ya ujenzi wa kiwanda hicho jijini Dar es Salaam yamekwishafanyika na kuonyesha hatua nzuri, hasa katika kipindi hicho ambacho serikali inahimiza ujenzi wa viwanda.
Tupia Comments: