Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kimekutana kujadili na kutoa msimamo wao juu ya mapendekezo ya Serikali kuanzisha Bodi ya Usajili wa Mawakili huku kikiwataka mawakili wake kusimamia maadili ya taaluma yao ili kutimiza majukumu kwa haki.

Akizumza kwenye mkutano huo Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema mapendekezo yaliyotolewa ni hatari kwa uhuru wa TLS na kada ya sheria kwa ujumla iwapo siasa itaingia kwenye kazi zao sheria.
Amesema bodi hiyo ikianzishwa itakuwa chini ya waziri wa sheria na katiba na ndiyo itakuwa na nguvu ya kusajili au kuwafuta wanasheria kadri itakavyoona inafaa.

"Mabadiliko haya ni hatari sana kwa uhuru wa wanasheria nchini, tumekutana hapa kuelezana na kupokea maoni ya wanachama kisha tutaweka msimamo wetu baada ya baraza la TLS kukaa Huo ni mkakati wa Serikali kuminya uhuru wa TLS ili kuwadhibiti wanasheria kuingia kwenye siasa, jambo ambalo  linatakiwa kupingwa na kila mtu kwa sababu matokeo yake ni mabaya" alisema Mh. Tundu Lissu.

Mbali na hayo Lissu amewaasa wanasheria kuwa endapo watashindwa kusimamia taaluma yao vizuri na kuruhusu siasa ikaingia ndani yake basi haitokuwa na maana ya  kuwepo kwa chama hicho.

Tupia Comments: