Maelezo juu ya kifo cha Seneta Mutula Kilonzo ambayo yanaendelea kujitokeza, yanapingana na ripoti ya Serikali ya Kenya ambayo ilitolewa siku ya Alhamisi.
Ripoti hiyo ilisema kuwa Kilonzo alikufa kutokana na kuvuja damu kwa wingi kutokana na shinikizo la damu.
Siku ya Alhamisi, Dkt S.W Mwangi ameiambia mahakama ya Machakos kuwa Kilonzo alishindwa kuamka kutoka usingizini na kuwa shinikizo la damu lilikuwa limezidi kiwango kutokana na kinywaji cha caffeine ambacho seneta huyo wa zamani alikunywa.
Barua pepe ambazo zilionekana na gazeti la Nation katika mabadilishano ya kiutalamu kati ya madaktari wachunguzi wa vifo wa Kenya na mwenzao huko Uingereza Ian Calder, ambaye alipewa shughuli hiyo ya uchunguzi na familia ya marehemu, inaonyesha simulizi tofauti kabisa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ambavyo viko karibu na Kilonzo vimesema alikuwa hajawahi kujulikana akinywa vinywaji venye kemikali ya carbonate au caffeine, “and asingeweza kunywa vinywaji kama hivyo hata kama ukimpa na hata akiwa na njaa ya namna gani”.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa huko Machakos muda mfupi Alhamisi, baada ya kuwa kimya kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu, na ilikuwa wiki mbili tu baada ya gazeti la nation kuhoji serikali wapi kesi hiyo ilikuwa imefikia.
Tupia Comments: