Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha video katika mtandao wa Twitter ikimuonyesha akimpiga mtu aliye na nembo kichwani ya shirika la habari la CNN.
Video hiyo iliyofanyiwa ukarabati ni ile inayomuonyesha Trump wakati alihudhuria michezo ya mieleka ya WWE mwaka 2007, ambapo ‘alimshambulia’ mmiliki wa michezo hiyo Vince McMahon.
Video hiyo inaonekana kuchapishwa katika mtandao yenye kumpendelea Trump mapema wiki hii. CNN baadaye ilimlaumu Rais kwa kuibua ghasia dhidi ya vyombo vya habari.
Mchambuzi mmoja katika kituo cha ABC, Ana Navarro, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Trump, alisema kuwa video hiyo ni uchochezi na huenda ikasababisha mwandishi kuuliwa.
Lakini mshauri wa masuala ya usalama nchini Marekani Thomas Bosset, ambaye awali alihojiwa na kituo cha ABC alisema video hiyo haionekani kuwa tisho.
Mara kwa mara Rais Trump amekuwa kwenye mzozo na kituo cha CNN anachokiita ‘taarifa bandia’
Tupia Comments: