Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo alimaarufu kama 'Mzee wa Upako' amefunguka na kusema mtu kufa maskini si jambo la kusifiwa hata kidogo kuwa ni uzalendo bali ni Ufala.
Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi cha UJENZI cha EATV kinachoruka kila Jumapili.
Mzee wa Upako anasema mtu anapokufa akiwa ameacha mali za kutosha ni jambo jema kwani familia yake nyuma haiwezi kupata taabu wala watoto hawawezi kupata shida tofauti na yule anayekufa akiwa na kitanda tu kwani watoto wake watapata shida na mateso.
"Watu wanamsifu mtu amekufa bila mali eti alikuwa mwadilifu yaani unakuta mtu amefanya kazi serikalini miaka na miaka, sijui miaka 35 au 40 anakufa hata kitanda hana.
"Wapo watu wanasema huyu jamaa alikuwa mzalendo na muadilifu sana hata kitanda hana, hamna mtu huyo alikuwa fala umenielewa?, huyu alikuwa fala na hastaili kuwa kielelezo cha msingi tuhoji mtu kapata mali wapi?
"Ndio jambo la msingi sababu unaacha watoto duniani unadhani wataishi vipi? Mama anakuwa na nyumba pale anachota kodi anapeleka watoto shule maisha yanaendelea" alisisitiza Mzee wa Upako.
Tupia Comments: