Wizara ya afya zanzibar imesema mwamko mdogo wa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kupatiwa matone ya vitamin A na chanjo ya dawa za minyoo katika vituo vya afya ni sababu inayopelekea watoto hao kuwakosesha haki zao za msingi na kusababisha wizara hiyo kutofikia malengo yao ya kutowa matibabu kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Malaria  Mwanakwerekwe ,Mkuu wa kitengo cha lishe Asha Hassan Salmin amesema mbali na jitihada mbali mbali wanazochukuwa Wizara ya Afya juu ya kutoa elimu ya kuihamasisha jamii kupeleka watoto wao katika vituo vya Afya lakini elimu hiyo hazifanyiwi kazi kama ilivyo kusudiwa .
Amesema kuwa tafiti zilizofanya  mwaka 2010 hadi 2016 zinaonyesha asilimia 12 ndio watoto wanaopatiwa vyakula vya vitamen A kutoka katika familia zao na walobaki zaidi ya asilimia 50 wamekuwa wakikosa Vitamin hivyo hali ambayo inawasababishia watoto kukosa kinga ya mwili kutokana na vyakula vya vitamin A na matone ya vitamin A yanayotolewa katika vituo vya afya.
Amesema sehemu zinazoongoza wazazi kutopeleka watoto kupatiwa matone hayo ni maeneo ya Mkoa wa Mjini Maghari ambapo mara zote hutowa idadi ndogo kinyume na matarajio yaliokusudia na kupelekea kujerejesha  nyuma jitihada za maafisa wa afya kuwafikishia wananchi huduma za afya hususani kwa watoto.
Aidha ametowa wito kwa wazazi na walezi kuwa na utamaduni wa Kuwapeleka watoto wao kupatiwa Matone ya vitamain A na chanjo ya minyoo  ili kuwakinga na maradhi yanayoweza kujitokeza ikiwemo ukosefu wa kinga katika mwili.

Tupia Comments: