Mataifa wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO pamoja na Canada yametangaza kuongeza kiwango cha fedha inachotumia kwa ulinzi kwa asilimia 4.3 mwaka huu wa 2017.
Katibu mkuu wa jumuiya hiyo Jens Stoltenberg amesema lengo hasa ni kuionyesha Marekani kwamba yamejitolea kugharamia zaidi.Ongezeko hilo linaonyesha kiwango cha juu kuwahi kutolewa na wanachama hao wa jumuiya ya NATO. Mwaka 2015 mataifa hayo yalitoa asilimia 1.8, huku mwaka uliopita kiwango cha fedha zinazotengewa ulinzi kikaongezwa kwa asilimia 3.3.Takwimu za kiasi cha fedha kitakachotolewa na kila taifa mwanachama zitatolewa kesho baada ya kuidhinishwa na mabalozi wa jumuiya ya NATO, lakini kwa ujumla matumizi ya mwaka huu yatakuwa dola billioni 280 na kuongezeka kwa dolla billioni 46 tangu kupunguzwa kwake,hali iliyoipunguzia uwezo muhimu bara la ulaya kwa mfano kuongeza mafuta ya ndege zake za kivita."Fedha hizo dola billioni 46 za Marekani zitatumika kwa mambo chungu nzima.Zitatumika katika uwekezaji mpya,matifa zaidi wanachama yanawekeza zaidi katika vifaa vipya,na pia kwa hakika zitatumika katika mazoezi zaidi, mishahara na pensheni amesema Stoltenberg.
Kwa mujibu wa Stoltenberg miongoni mwa mataifa 27 wanachama wa NATO ni manne tu, Ugiriki, Uingereza, Poland na Estonia yaliyochangia kiwango cha fedha yanayohitajika mwaka 2016. Romania itatimiza kiwango hicho mwaka huu huku Latvia na Lithuania zikifanya hivyo mwaka ujao wa 2018."Ili kuweka mataifa yetu salama, tunahitaji kuendelea kujitahidi kuongeza fedha zinazotengewa ulinzi na kugawana mzogo huo miongoni mwa mataifa wanachama.Tumeanza kuchukua mkondo sahihi na hii leo naweza kutangaza maendeleo makubwa zaidi.
Bulgaria na Romania zapinga vikwazo dhidi ya Urusi
Maafisa wa NATO wamesisitiza kuwa wakati msimamo mkali wa rais wa Marekani Donald Trump ulifanya kupigwa darubini matumizi ya ulinzi,vitendo vya Urusi kuliyakua jimbo la Ukraine la Crimea mwaka 2014 vilikuwa na athari zaidi huku mataifa wanachama kwa pamoja yakikubaliana kutopunguza matumizi yao. Kwa upande mwengine, marais wa Bulgaria na Romania wamesisitiza kuwa hawaipingi Urusi,licha ya mataifa hayo mawili ya mashariki mwa ulaya kuwa wanachama wa NATO na Umoja wa ulaya. Umoja wa ulaya ulikubaliana kuiongezea vikwazo Urusi kuhusiana na vitendo vyake nchini Ukraine .Rais wa Bulgaria Ruemen Radev amesema mawasiliano na Urusi yapaswa kuwekwa wazi,ili kuwepo majadiliano yatakayopunguza mvutano na kuepuka hatari zinazoweza kutokea. Bulgaria ni miongoni mwa wanachama maskini zaidi wa Umoja wa ulaya na inategemea sana gesi kutoka Urusi.
Tupia Comments: