Serikali wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imewataka wananchi wote waliokuwa na dhamira ya kwenda kuvamia sehemu za machimbo ya madini kwa kisingizio kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli amewaruhusu waache kufanya hivyo mara moja.

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu  ameyasema hayo leo, kufuatia taarifa ya tume ya pili ya rais ilyofuatilia athari za usafirishaji nje wa mchanga wenye dhahabu (makinikia), iliyotolewa juni,12 mwaka huu jijini Dar-es-salaam.

Nkurlu amesema serikali imebaini kuwepo kwa tetesi za watu wachache kujipanga kwenda kuvamia sehemu zinazomilikiwa na wawekezaji wa migodi hususan ACACIA na Nyang’hwale kwa madai kwamba rais Magufuli ameruhusu, jambo ambalo siyo kweli.

Amesisitiza alichokielekeza rais Magufuli ni kwamba uzalishaji migodini unaendelea kama kawaida chini ya usimamizi na udhibiti wa serikali na wala siyo vinginevyo.


Tayari Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation Profesa John Thonton amekutana na Rais Dkt John Pombe Magufuli, ambapo amekubali kuwa kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Tupia Comments: