Kabla ya ujio wa Lowasa na kuondoka kwa Dr. Slaa, Chadema kilikuwa kinaongoza mijadala kuhusu mstakabali wa nchi yetu. Chadema walifanikiwa ku-plan strategically mijadala na mikakati ya kisiasa nchini na hivyo kuwafanya CCM kuwa katika defensive mode (kujihami). CCM kilipata ganzi ya akili na hivyo kazi yao ilikuwa kuwasubiri CDM waibue mijadala na hivyo CCM kuwa reactive.

Mambo yaligeuka kabisa tangu helikopita ilipogiga reverse angani. That was a defining moment ambapo CDM ilianza kuwa reactive. Harakati za vijana wa CDM, ambao walikifanya chama kupendwa kwa hoja zao mruwa zikafifishwa. Akatangulizwa Lowasa badala ya vijana hawa akina Mdee, Mnyika, Msigwa, Lissu, n.k. Wengi tulitahadharisha sana na kuwaonya CDM kuwa Lowasa atakuwa liability (mzigo) kwa chama. Tuliona kuwa viongozi wa CCM walikuwa pre-occupied na matokeo ya muda mfupi waliyodhani watayapata, badala ya kuendelea kujenga taasisi endelevu -yenye mizizi mpaka chini kabisa katika mioyo ya watu. CDM inayoongozwa na vijana na yenye kuongoza mijadala yakisiasa Tanzania. Tulionya kuwa nafasi na harakati za vijana, pamoja na ajenda ya CDM ya kupinga ufisadi zitazimuliwa kama siyo kuzimwa kabisa. Ndicho kilichotokea.



Kabla ya kuendelea ngoja nitoa ufafanuzi wa tofauti ya neno reactive na proactive:
Ukiangalia kwenye dictionary na maelezo mbalimbali kutoka kwenye mitandao utaona tofauti zifuatazo za maneno haya mawili.

Reactive: done in response to a problem or situation : reacting to problems when they occur instead of doing something to prevent them. A person who is reactive usually responds to another, but does not act on himself. Such people do not usually take the initiative in something. This is a negative feature of an individual as the person. People who are reactive in society need a push to complete a task. They do not take it upon themselves unless they are being told to by someone else.

Proactive: refers to being prepared even before an incident takes place. A proactive person takes the initiative and is prepared, unlike a reactive person. Unlike a reactive leader who responds to situations as and when events take place, a proactive leader is one who anticipates what is going to happen and works accordingly to minimize the effect of the event or to work to take advantage of the event.

CCM wame-take advantage ya ujio wa Lowasa na Sumaye CDM. Kwa mfano hivi karibuni, katika Bunge Chadema walipendekeza kuwa marais waliohusika kwa namna moja ama nyingine kuwepo kwa mikataba nyonyaji ya madini kati ya nchi yetu na wawekezaji (wanyonyaji au wezi kama wengine wanavyowaita) nao washughulikiwe. Ndugai aliwaambia CDM kuwa wawe makini na wakumbuke CDM wana viongozi wawili wanaohusika na maamuzi ya mikataba, akimaanisha Lowasa na Sumaye. Kumbe hapa Ndugai anakuwa kama wale wanaotumia mbinu yak u-blackmail. Anakuhusisha katika jambo chafu halafu anatumia weakness hiyo kukuendesha na kukutumia kama anavyotaka. CDM wanyea.

Nini kifanyike ndani ya CDM?

Wakati wa changamoto za kisiasa kama sasa ambapo serikali inaminya demokrasia ya vyama vingi, ni wakati wa CDM kuwa wabunifu zaidi. Wanatakiwa wafanye yafuatayo kwa haraka sana.

1. Lowasa na Sumaye wasiwekwe forefront katika harakati za kisiasa za CDM. Wawekwe nyuma ya pazia, wasionekane. Hawa si symbol ya harakati za CDM. Wakati ukifika CDM iwa-phase out.

2. Vijana warudi forefront kama tunavyoijua CDM. Alama ya harakati za CDM iwe vijana wakiwemo akina Mnyika, Msigwa, Vincent Nyerere, Halima Mdee, Lissu n.k.

3.CDM ya akina Baregu, Safari n.k. (huku Lowasa na Sumaye wakiwekwa nyuma ya pazia- tena mbali kabisa) wabuni strategy za kisiasa na mijadala ya kisera ili CCM irudi mahali pake pa kuwa reactive na defensive na CDM wawe proactive na hivyo kuwa viongozi katika nchi hii.

Tupia Comments: