Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ametoa onyo dhidi ya Korea Kaskazini kupitia mtandao wa twitter, akisema kuwa Pyongyang inatafuta matatizo.
Pia aliitaka China ambayo ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kujaribu kukabiliana na jirani wake huyo.
Bwana Trump alipendekeza kuwa China itapata makubaliano bora ya kibiashara ikiwa itafanya hivyo, lakini akaongeza kuwa Marekani haitaogopa kutatua tatizo la Korea Kaskazini bila ya Uchina.
Bwana Trump alitoa matamshi kama hayo wiki moja iliyopita lakini tangu wakati huo msukosuko umekuwa mkubwa.
Marekani imetuma meli za kivita kuenda kwa maji ya rasi ya Korea hatua ambayo imeighadhabisha Korea Kaskazini.
Tupia Comments: